Kids Education – YGTF https://yatimagrouptrustfund.co.tz Yatima Group Trust Fund Sat, 11 May 2024 12:20:31 +0000 en-US hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.6.1 TAASISI YA THE HOPE CAMPAIGN YATOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA CHAMAZI https://yatimagrouptrustfund.co.tz/2023/05/23/taasisi-ya-the-hope-campaign-yatoa-msaada-kwa-watoto-yatima-chamazi/ https://yatimagrouptrustfund.co.tz/2023/05/23/taasisi-ya-the-hope-campaign-yatoa-msaada-kwa-watoto-yatima-chamazi/#respond Tue, 23 May 2023 17:56:29 +0000 https://thememxpro.com/theme/sopot/?p=1167
TAASISI ya The Hope Campaign imetoa msaada wa vyakula na vifaa vya shuleni kwa Kituo cha Yatima Group Trust Fund cha Chamazi Temeke jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kukabidhi msaada huo kituoni hapo, Mratibu wa Taasisi hiyo Mpelo Kapama alisema msaada huo umelenga kuwasaidia watoto hao kwa ajili ya chakula na vifaa vya kusomea.
IMG_0291
Hapa ni kikosi kamili cha taasisi hiyo kabla ya kukabidhi msaada huo.

“Taasisi yetu kupitia kwa mwezeshaji wetu mkuu John Amigo imejijengea utamaduni wa kusaidia makundi mbalimbali yenye uhitaji kama watoto hao na kambi za ukimbizi na mara nyingi tumekuwa tukisaidia kituo hiki” alisema Kapama.

Katibu wa Kituo hicho cha Yatima, Fred George alisema ni muhimu kwa jamii kujitokeza kusaidia Yatima na kuwafariji kama ilivyofanya taasisi hiyo.

Alisema kituo hicho chenye watoto zaidi ya 150 kimekuwa na changamoto ya chakula, fedha za kuwalipa wafanyakazi pamoja na ujenzi wa uzio kwa ajili ya usalama.IMG_0236Mratibu wa Taasisi ya The Hope Campaign, Mpelo Kapama (kushoto), akiwaelekeza maofisa wenzake kabla ya kwenda kukabidhi msaada huo.
IMG_0246Mizigo ikitolewa kwenye gari.
IMG_0253Aman Issaya wa taasisi hiyo akiwa na kiroba cha sukari akielekea eneo la makabidhiano.
IMG_0256
Mratibu wa Taasisi ya The Hope Campaign, Mpelo Kapama, akiwa amebeba kiroba cha sukari wakati taasisi hiyo ilipotoa msaada wa vyakula na vifaa vya shuleni kwa Kituo cha Yatima Group Trust Fund cha Chamazi Temekie jijini Dar es Salaam leo.
IMG_0258
Vifaa hivyo viwekwa sawa kabla ya kukabidhi.
IMG_0264
Aman Issaya wa taasisi hiyo (kushoto), akimkabidhi Katibu Mkuu wa Kituo hicho, msaada huo. Kulia ni Mratibu wa Taasisi ya The Hope Campaign, Mpelo Kapama na Furaha Kapama.
IMG_0269Furaha Kapama (kushoto), akimkabidhi msaada Katibu Mkuu wa Kituo hicho, Fred George.
IMG_0273
Upendo Kapama akikabidhi msaada huo.
IMG_0276 

Thomas Anzuluni akimkabidhi Katibu wa kituo hicho, Fred George msaada wa mafuta ya kula.
IMG_0280
Mwakilishi wa Taasisi ya The Hope Campaign, Stela Mpelo (kushoto), akiwakabidhi vifaa vya shule watoto Yatima wa Kituo cha Yatima Group Trust Fund cha Chamazi Temeke jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Ofisa wa taasisi hiyo, Thomas Anzuluni na Katibu wa kituo hicho, Fred George.
IMG_0285Aman Issaya wa taasisi hiyo (kushoto), na Katibu Mkuu wa Kituo hicho wakiwa wameshika mipira iliyotolewa na taasisi hiyo kwa watoto wa kituo hicho.
IMG_0300
Ni pozi la kukata na shoka na vipeperushi mkononi. Na Dotto Mwaibale
]]>
https://yatimagrouptrustfund.co.tz/2023/05/23/taasisi-ya-the-hope-campaign-yatoa-msaada-kwa-watoto-yatima-chamazi/feed/ 0